Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya watu 35 wapoteza maisha ghala la mafuta likiteketea Benin

Moto Ghalaaa Ghalaaa.jpeg Zaidi ya watu 35 wapoteza maisha ghala la mafuta likiteketea Benin

Sun, 24 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

makumi ya watu wameripotiwa kuuawa nchini Benin baada ya ghala la mafuta kulipuka na kuababisha moto na wingu jeusi la moshi angani katika mji wa Seme-Podji karibu na mpaka na Nigeria.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Benin amesema moto huo ulitoke jana Jumamosi kwenye ghala la mafuta ya magendo katika mji wa Seme-Podji kusini magharibi mwa mwa nchi hiyo. Alassane Seidou amesema watu wasiopungua 35 wameaga dunia kutokana na mlipuko huo wakiwemo vichanga wawili.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Benin ameongeza kuwa "sababu ya moto huo ni mafuta ya magendo". Amesema moto huo umeteketeza vibaya miili ya waathiriwa."

Mwendesha Mashtaka wa Benin, Abdoubaki Adam-Bongle amesema: Moto umeteketeza duka la mafuta ya magendo na kulingana na tathmini ya awali umesababisha vifo vya watu 35."

Zaidi ya dazeni ya wengine wamejeruhiwa vibaya na wanapatiwa matibiwa hospitalini.

Magendo ya mafuta ni jambo la kawaida katika mpaka wa Benin na Nigeria, ambayo ni mzalishaji mkuu wa mafuta. Viwanda haramu vya kusafisha mafuta, dampo za mafuta na mabomba vimetengenezwa kinyume cha sheria katika miji ya mpakani, na wakati mwingine husababisha moto na maafa.

Wizara ya Sheria ya Benin imetangaza kuwa imeanzisha uchunguzi wa tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live