Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya watu 100 wameripotiwa kufariki ajali ya boti Congo

Drcnn Zaidi ya watu 100 wanakadiriwa kufariki ajali ya boti Congo

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watu 100 wanasadikika kupoteza maisha katika ajali ya boti iliyotokea katika mto Congo uliopo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Nae msemaji wa gavana wa Mkoa wa Kaskazini Magharibi eneo ambalo ajali hiyo ilitokea Nestor Magbado, amesema kuwa hadi sasa Jumla ya miili 51 tayari imeshapatikana huku miili 69 ikiwa bado haijapatikana.

Ajali hiyo ilitokea Oktoba 05,2021 na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji huyo inaeleza kuwa hadi sasa jumla ya watu waliokolewa wakiwa hai ni 39 pekee.

Hata hivyo Msemaji huyo amesema kuwa hakuna uthibitisho wa idadi kamili ya abiria waliokuwa kwenye kivuko hicho ila kwa makadirio yaliyofanywa na mamlaka za uokoaji yametoa idadi hiyo ya watu 100 kwa kuzingatia uwezo wa boti hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live