Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya watu 100 wafa kwa kipindupindu, dengue Sudan

Kipindupindu Chasababisha Vifo Vya Watu 10 Afrika Kusini Zaidi ya watu 100 wafa kwa kipindupindu, dengue Sudan

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya ya Sudan imesema tokea mwezi August zaidi ya watu 100 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kipindupindu na dengue katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita.

Wizara hiyo imeongeza kuwa kati ya jumla ya visa 1,049 vya ugonjwa wa kipindupindu, 73 kati yake vimesababisha vifo mjini Khartoum, katika Jimbo la Al-Jazira Kusini na Jimbo la Gedaref upande wa magharibi mwa nchi hiyo.

Khartoum imekuwa uwanja wa mapigano makali kati ya wafuasi wa majenerali hasimu, ambayo yameikumba nchi hiyo tokea mwezi Aprili.

Mamia ya maelfu ya wakaazi wa Khartoum wamekimbilia maeneo ya utulivu ya Gedaref na Al-Jazira, na kupelekea maeneo hayo kukabiliwa na uhaba wa maji safi ya kunywa.

Wizara ya Afya ya Sudan pia imesema majimbo tisa ya Sudan yamerekodi visa vya maradhi ya dengue yanayoenezwa na mbu, ambapo vifo 49 vimerikodiwa kati ya visa 3,316. Hali ya Sudan

Jimbo la Gedaref, ambalo linapakana na Ethiopia, limeripoti kesi 2,152 na vifo 33.

Hata kabla ya kuanza mapigano mwezi Aprili, mfumo wa huduma za afya nchini Sudan ulikuwa umezorota na hivyo kuandaa uwanja wa kuzuka magonjwa ambayo huambatana na msimu wa mvua ambao huanza mwezi Juni nchini humo.

Hivi sasa mfumo wa afya nchini humo unakabiliwa na hali tata kwa kulengwa hospitali kwa mabomu, kupungua dawa na huduma za afya pamoja na madaktari wengi kukimbia nchi.

Ripoti ya Wizara ya Afya inasema asilimia 70 ya hospitali katika maeneo ya vita hazitoi huduma yoyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live