Zaidi ya wanawake 42 wametekwa nyara na wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali kaskazini mashariki mwa Nigeria ambako waasi waliwashambulia wanawake hao walipokuwa wakikusanya kuni katika wilaya ya Jere jimbo la Borno ambalo ni kitovu cha uasi.
Zaidi ya wanawake 42 wametekwa nyara na wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali kaskazini mashariki mwa Nigeria ambako waasi waliwashambulia wanawake hao walipokuwa wakikusanya kuni katika wilaya ya Jere jimbo la Borno ambalo ni kitovu cha uasi. Inaelezwa kuwa wahanga wa utekaji huo walikuwa wanatoka katika kambi ya wakimbizi wa ndani katika wilaya jirani ya Mafa na wamekuwa wakiuza kuni ili kujikimu kimaisha, huku hali ngumu ya kiuchumi nchini ikizidi kuongezeka.