Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya wanawake 30 watekwa nyara Cameroon

Zaidi Ya Wanawake 30 Watekwa Nyara Na Watu Wanaotaka Kujitenga Cameroon Zaidi ya wanawake 30 watekwa nyara Cameroon

Wed, 24 May 2023 Chanzo: Voa

Wapiganaji wanaotaka kujitenga katika eneo la kaskazini-magharibi lenye machafuko nchini Cameroon wamewateka nyara zaidi ya wanawake 30 na kujeruhi idadi isiyojulikana ya wengine, maafisa wamesema.

Wanawake hao walitekwa nyara katika kijiji cha Big Babanki, karibu na mpaka na Nigeria, kwa madai ya kupinga amri ya kutotoka nje na kutozwa kodi na watu wanaotaka kujitenga.

"Takriban wanawake 30 walitekwa nyara na watu wanaotaka kujitenga [Jumamosi asubuhi] - bado hatujawapata," kanali wa jeshi aliliambia shirika la habari la AFP.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini vinaripoti kuwa idadi ya waliopotea ilikuwa kubwa zaidi - hadi wanawake 50.

Maafisa walisema baadhi ya wanawake "waliteswa vikali" na waasi waliojihami vikali, ambao mara kwa mara huwateka nyara raia, hasa kwa ajili ya fidia.

Kiongozi wa wanaotaka kujitenga Capo Daniel aliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba wanawake hao wanaadhibiwa kwa kuruhusu "kudanganywa" na serikali ya Cameroon.

Jeshi linasema kuwa limetuma wanajeshi kuwakomboa wanawake hao.

Cameroon imekuwa ikikumbwa na mapigano tangu watu wanaotaka kujitenga wanaozungumza Kiingereza waanzishe uasi mwaka 2017.

Mzozo huo umegharimu maisha ya zaidi ya watu 6,000 na kuwalazimu zaidi ya watu milioni moja kukimbia makazi yao, kulingana na Kundi la Crisis.

Chanzo: Voa