Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya wananchi milioni 18 wamejitokeza kupiga kura Morroco

Morokoo Uchaguzi mkuu Morroco waanza leo

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi nchini Morroco, wameanza mchakato wa kupiga kura ikiwa ni haki yao kikatiba ya kuwachagua viongozi watakao waongoza nchini humo.

Taarifa zinaeleza kuwa vituo vya kupigia kura vimefunguliwa kuanzia saa 08:00 asubuhi na vitakuwa wazi hadi saa 19:00 usiku ili kuwapa nafasi wananchi kushiriki zoezi hilo litakalo amua hatma ya uongozi wa chama tawala cha Islamist PJD, kinachoongoza kwa miongo mingi.

Takribani wapiga kura milioni 18 wanatarajiwa kupiga kura ikiwa ni idadi kubwa kutokea kulinganisha chaguzi zilizopita, huku wanaogomea ubunge wakiwa ni 395 na zaidi ya wagombea 31,00 wakiwa wanagombea uwakilishi wa serikali za mtaa pamoja na Mkoa.

Inaelezwa kuwa Kiongozi mkuu wa serikali katika nchi hiyo yenye utawala wa kifalme, hutoka katika chama kilichoshinda uwakilishi bungeni kwa kuchaguliwa na mfalme wao ili kuunda baraz litakalo tawala kwa miaka mitano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live