Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya wakimbizi 1,000 kutoka DRC waingia Uganda

Wakimbizi Drc Drc.jpeg Zaidi ya wakimbizi 1,000 kutoka DRC waingia Uganda

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya wakimbizi 1,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamekimbilia Uganda kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni ya waasi wanaoshukiwa kuwa wa Allied Democratic Forces (ADF).

Shirika la Msalaba Mwekundu la Uganda (URCS) kimetangaza habari hiyio na kuongeza kuwa, wakimbizi hao wameingia Uganda kupitia wilaya ya mpakani ya Bundibugyo ya Mkoa wa Magharibi wa Uganda.

Irene Nakasiita, msemaji wa URCS amesema: "Maafisa wa Wilaya ya Bundibugyo wametangaza kuwa, wamewapa hifadhi wakimbizi hao katika Kituo cha Usafiri cha Bubukwanga ili kuruhusu serikali na washirika wengine kutoa msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi hao." Rais wa kawaida ndio wahanga wakuu wa machafuko

Ameongeza kuwa, wakimbizi hao wapya wamesajiliwa kama ilivyo utaratibu, na kwa upande wake,Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Uganda URC limetoa huduma ya kwanza ya haraka kwa waliojeruhiwa na baadaye kuwapeleka kwenye kituo cha afya cha eneo hilo kwa huduma zaidi.

Aidha amesema: "Tunaunga mkono juhudi za kuhakikisha wakimbizi hao wanarejeshwa kwenye familia zao hasa watoto ambao hawakuandamana na familia zao kutokana na hamkani ya kukimbilia usalama wao baada ya kuzuka mashambuilzi hayo."

Tangu mwaka wa 2022, operesheni ya pamoja ya kijeshi iliyohusisha vikosi vya Jeshi la Taifa la Uganda UPDF na vile vya DRC imekuwa ikiwasaka waasi wa Uganda wa ADF, wanaotumia ardhi ya Kongo kufanya mashambulio ya kigaidi.

Uganda ina wakimbizi wasiopungua milioni 1.5 wengi wao ni kutoka DRC, Sudan Kusini, Rwanda, Burundi, Eritrea na Somalia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live