Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya wahamiaji haramu 17,000 waliokolewa katika pwani ya Libya mwaka 2023

Wahamiaji Watoto Wanachukuliwa Kama Watu Wazima Uhispania Zaidi ya wahamiaji haramu 17,000 waliokolewa katika pwani ya Libya mwaka 2023

Wed, 3 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kuwa, wahamiaji haramu 17,025 waliokolewa na kurudishwa Libya kuanzia mwezi Januari hadi Disemba, 2023.

Katika ripoti yake ya kila mwaka, shirika la IOM pia limesema kuwa, wahamiaji 974 walikufa na 1,372 walipotea kwenye Bahari ya Mediterania katika pwani ya Libya mwaka 2023.

Libya imekuwa njia kuu inayotumiwa na wahamiaji haramu kutokana na kukosekana na serikali kuu tangu ulipoangushwa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011. Wengi wa wahamiaji hao haramu ni raia wa nchi za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara na wanahatarisha maisha yao kwa tamaa chapwa za kupata maisha mazuri barani Ulaya.

Hii ni katika hali ambayo tarehe 19 Novemba mwaka ulioisha wa 2023, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji lilitangaza kuwa, katika kipindi cha wiki moja tu lilikuwa limeokoa wahamiaji haramu 662 katika pwani za Libya.

Taarifa hiyo ilisema kuwa, baina ya Novemba 12 na 18, 2023, wahamiaji 662 walikamatwa na kurejeshwa Libya.

Wahamiaji haramu wengi wanatoka katika nchi za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara

Wakati huo shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilisema kuwa, hadi mwezi Novemba, wahamiaji haramu 14,894 walikuwa wameshaokolewa na kurudishwa Libya, 940 walikuwa wameshakufa na 1,248 walikuwa hawajulikani wamepotelea wapi katika jitihada zao za kujaribu kuvuka mawimbi makubwa ya Bahari ya Mediretenia kuelekea barani Ulaya.

Mwezi Septemba 2023 pia, serikali ya Libya ilianzisha operesheni ya kuwafukuza na kuwarejesha makwao wahamiaji haramu waliozuiliwa nchini humo wakati walipokuwa wanajaribu kuelekea barani Ulaya.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Libya, Emad al-Tarabelsi alisema kuwa, ndege kadhaa zitatumika kuwasafirisha wahamiaji 270 kutoka Tripoli hadi kwenye nchi zao za asili ambazo ni Somalia, Sudan, Nigeria na Bangladesh.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live