Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya wahamiaji 60 wanahofiwa kufa maji kutoka Libya

Zaidi Ya Wahamiaji 60 Wanahofiwa Kufa Maji Kutoka Libya Zaidi ya wahamiaji 60 wanahofiwa kufa maji kutoka Libya

Sun, 17 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Zaidi ya wahamiaji 60 wanaaminika kufa maji katika ajali ya meli katika pwani ya Libya, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema.

Likinukuu manusura, shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilisema Jumamosi meli hiyo iliondoka katika mji wa Zuwara ikiwa na takriban watu 86.

Ilisema mawimbi makubwa yaliikumba mashua hiyo na kwamba wahamiaji 61, wakiwemo watoto, hawakupatikana na kudhaniwa kuwa wamefariki.

Libya ni miongoni mwa sehemu kuu za kuondoka kwa wahamiaji wanaojaribu kuvuka bahari ya Mediterania na kuingia Ulaya.

IOM inakadiria kuwa zaidi ya watu 2,200 wamekufa maji walipokuwa wakijaribu kuvuka mwaka huu pekee, na kuifanya kuwa mojawapo ya njia hatari zaidi za uhamiaji duniani.

Shirika hilo lilisema wengi wa wahanga wa tukio la hivi punde zaidi walikuwa kutoka Nigeria, Gambia, na nchi nyingine za Afrika, shirika la habari la AFP linaripoti.

Pia imesema manusura 25 wamehamishiwa katika kituo cha kizuizini nchini Libya na walikuwa wakipatiwa msaada wa kimatibabu.

Chanzo: Bbc