Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya wahamiaji 1,200 waokolewa Bahari ya Mediterania

A9CA1B41 816C 4FCF A220 E57489B66A68 W1200 R1 Zaidi ya wahamiaji 1,200 waokolewa Bahari ya Mediterania

Wed, 27 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya wahamiaji 1,200 waliokolewa katikati ya bahari ya Mediterania siku chache zilizopita hali tulivu ya bahari iliwawezesha kuvuka kutoka Afrika Kaskazini kwenda Ulaya.

Operesheni mbalimbali za uokoaji zilifanywa na mashirika ya misaada ya Kimataifa Kama walinzi wa Pwani ya Italia na Meli mbalimbali za kibiashara.

Vyombo vya Italia vimepata miili ya watu watano na kuokoa takribani watu 674. Walinzi wa Pwani wa Italia walisema jumapili, huku mashirika mbalimbali ya Ulaya yakiripoti kuokoa zaidi ya watu 500.

Baadhi yawalionusurika walilazimika kung’olewa kutoka baharini Katika operesheni ya Italia jumamosi, ambayo ilifanywa kwa maili 120 (190 kilomita) kutoka pwani ya kalabria na meli za kibiashara pamoja na Boti tatu za doria za walinzi wa Pwani.

Idadi ya wahamiaji waliofikia Italia imeongezeka kwa takribani robo moja kutoka 2021, na kufikia 34,013 siku ya ijumaa.

Idadi iko chini katika kilele cha mwaka 2015,l akini imesalia kuwa mbaya huku watu 1,234 wakiripotiwa kufariki dunia au kupotea baharini na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live