Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya wafungwa 1,800 wametoroka gerezani nchini Nigeria

Aa44082cabc83ee6 Zaidi ya wafungwa 1,800 wametoroka gerezani nchini Nigeria

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Wafungwa 1,844 wametorka gerezani baada ya watu waliojihami kwa bunduki na vilipuzi kuwavamia

- Kati ya 1,844 hao, sita wameripotiwa kurejea na wengine 35 hawakufanikiwa kutoroka

- Rais Muhammadu Buhari amewaagiza maafisa wa polisi kuwasaka wafungwa hao na kuwakamata tena haraka iwezekanavyo

- Buhari pia ametaka waliotekeleza shambulio hilo wakamatwe na wakabiliwe vilivyo kisheria

Maafisa wa polisi nchini Nigeria wameripoti kuwa zaidi ya wafungwa 1,800 wametoroka gerezani baada ya watu waliojihami kwa bunduki kuvamia gereza moja lililopo Mashariki mwa Owerri.

Kwa mujibu wa taarifa za BBC, washambuliaji hao walikuwa pia wamejihami kwa vilipuzi, wafungwa sita wamerejea gerezani kufika sasa huku 35 wakikataa kutoroka.

Polisi wamelaani kisa hicho huku wakilaani kundi moja ambalo linasemekana kupanga njama ya kujitenga na wenyeji wa Biafra, hata hivyo kundi hilo limepinga vikali madai hayo.

Msemaji wa polisi nchini humo ameambia vyombo vya habari kwamba, washambuliaji hao walitumia maroketi, maguruneti na silaha nyinginezo katika uvamizi huo, hakuna maafa yalioripotiwa.

Akitoa taarifa yake kwa umma, Rais Muhammadu Buhari amelitaja shambulio hilo kuwa la kigaida na ametaka waliolitekeleza wakabiliwe vikali kisheria watakapokamatwa.

Rais Buhari pia amewaagiza maafisa wa polisi kuwasaka na kuwakamata wafungwa waliotoroka kwenye gereza hilo.

Msemaji wa vuguvugu la watu Biafra amekanusha vikali madai kwamba kundi hilo lilihusika kwenye shambulio hilo kabisa.

Imeripotiwa kwamba tangu mwezi Januari mwaka huu, vituo kadhaa vya polisi hasa katika eneo la Kusini Mashariki mwa Nigeria yamekuwa yakishambuliwa na silaha kama bunduki kuibiwa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke