Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya tani 3.25 za bangi zakamatwa Morocco

Shamba La Bangi Zaidi ya tani 3.25 za bangi zakamatwa Morocco

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vyombo vya usalama vya Morocco vimetangaza kuwa vimefanikiwa kukamata zaidi ya tani 3.25 za bangi katika Bandari ya Tangier-Med na kumtia mbaroni mtu mmoja akihusishwa na magendo hayo.

Katika taarifa yake ya jana Jumatatu, Jeshi la Polisi la Morocco limetangaza kuwa, maafisa wa jeshi hilo na wafanyakazi wa forodha wamefanikiwa kukamata kiwango hicho kikubwa cha bangi iliyokuwa kwa sura ya utomvu uliobanikwa, ikiwa imefichwa ndani ya trela ya lori lililokuwa linasafirisha shehena ya samaki kuelekea nchini Uhispania.

Dereva wa lori hilo ambayo ni mwanaume raia wa Morocco mwenye umri wa miaka 32, amekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi ili kulisaidia jeshi la polisi kugundua mtandao au mitandao yote inayofanya kazi kimataifa katika magendo ya mihadarati na madawa haramu ya kulevya.

Serikali ya Morocco inadai kuwa inafanya juhudi kubwa hasa miaka 10 iliyopita kupambana na mihadarati na ukulima wa banti lakini Morocco imeendelea kuwa moja ya nchi zinazozalisha bangi kwa wingi duniani. Bangi ni haramu lakini dunia imeshindwa kupambana nayo

Miongozi mwa kiwango kikubwa zaidi cha bangi kilichogunduliwa nchini Morocco ni kile cha mwezi Oktoba, 2020 waka maafisa wa nchi hiyo walipotangaza kuwa wamefanikiwa kukamata tani 5.6 za bangi katika operesheni mbili tofauti zilizofanyika nchini humo.

Shirika rasmi la habari la Morocco MAP lilitangaza habari hiyo na kuwanukuu maafisa wa serikali wakisema kuwa, askari wa Kikosi cha Gadi ya Fukwe cha Morocco, walifanya doria katika ufukwe wenye ukubwa wa kilomita 4 magharibi mwa mji wa al Hoceima wa kaskazini mwa nchi hiyo na kukamata mafurushi 117 ya bangi yenye uzito wa tani hizo nyingi za madawa ya kulevya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live