Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya raia 130 wauawa na waasi wa DR Congo - UN

Zaidi Ya Raia 130 Wauawa Na Waasi Wa DR Congo   UN Zaidi ya raia 130 wauawa na waasi wa DR Congo - UN

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Umoja wa Mataifa unasema maelezo yametolewa kuhusu mauaji ya watu wengi mwishoni mwa Novemba mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mikononi mwa waasi wa M23.

Inasema uchunguzi umethibitisha vifo vya takriban raia 131 katika vijiji viwili - Kishishe na Bambo - katika wilaya ya Rutsuhuru mkoani Kivu Kaskazini.

Umoja wa Mataifa unasema wahasiriwa walinyongwa katika kile kinachoonekana kuwa kulipiza kisasi mashambulizi ya sasa ya serikali.

Hata hivyo, waasi wa M23, ambao wameteka miji kadhaa karibu na mpaka wa Rwanda na Uganda mwaka huu, wamekanusha kuwa wanashambulia raia

Chanzo: Bbc