Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya dola milioni 71 kukarabati jengo la Bunge lililoungua

Kuungua Jengooo Zaidi ya dola milioni 71 kukarabati jengo la Bunge lililoungua

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kujengwa upya sehemu za Bunge la Afrika Kusini ambazo ziliharibiwa na moto mapema mwaka huu kutagharimu zaidi ya Rand bilioni 1.2 sawa na dola za Kimarekani milioni 71.06.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi wa Umma na Miundombinu wa Afrika Kusini, Bi Patricia de Lille ambaye ameongeza kwa kusema, ripoti ya mwisho kuhusu tukio hilo imepelekwa kwa Spika wa Bunge na Mamlaka ya Mashtaka ya Taifa (NPA).

Tarehe 2 Januari mwaka huu, moto uliteketeza Majumba ya Bunge huko Cape Town na kusababisha uharibifu mkubwa kwa jengo hilo.

Mshukiwa alikamatwa kuhusiana na moto huo, na anakabiliwa na mashtaka kadhaa yakiwamo ya kuvunja nyumba kwa nia ya kufanya ugaidi pamoja na makosa mawili ya kuchoma moto na wizi.

"Ni zaidi ya R bilioni 1.2, hiyo ndiyo gharama inayokadiriwa na Shirika la Maendeleo, mara tu bunge litakapoamua kuunda upya sehemu ya ndani ya Bunge," de Lille amesema.

Katika jengo hilo kunahifadhiwa maelfu ya hazina zenye thamani kubwa vikiwemo vitabu vya kihistoria, picha na kazi muhimu za sanaa.

Majengo ya Bunge hilo yana sehemu tatu kuu, huku sehemu ya kale zaidi ikiwa ni ile iliyojengwa mwaka 1884. Sehemu mpya zaidi ni ile iliyojengwa mwaka 1980 ni ndilo Bunge la Taifa na nyingine ilijengwa mwaka 1920.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live