Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yvonne Chaka Chaka azungumzia kutimuliwa Uganda

90634 Vyone+pic Yvonne Chaka Chaka azungumzia kutimuliwa Uganda

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mkongwe wa muziki Afrika, Yvonne Chakachaka amekanusha kufukuzwa nchini Uganda, licha ya msemaji wa Jeshi la Polisi nchini humo, Fred Enaga kueleza wamefanya hivyo.

Chakachaka alikuwa Uganda kwa ajili ya kufanya shoo siku ya mkesha wa mwaka mpya juzi Jumanne Desemba 31, 2019 lakini hakufanya hivyo baada ya kutakiwa kuondoka kutokana na kutokuwa na kibali cha kufanya kazi.

Msemaji wa Jeshi la Poilisi la Uganda  Fred Enanga alisema, “tumemalizana na msanii huyo lengo ni kuhakikisha kunakuwa na ukweli katika kufuata kanuni na taratibu za mamlaka ya uhamiaji kwa watu wote wanaotutembelea nchini mwetu.”

“Tuna matumaini Chaka Chaka  atakapohitaji kuja tena hapa nchini atakusanya nyaraka sahihi kwa ajili ya kutumbuiza,” alisema Enanga.

Lakini Chakachaka ameviambia vyombo vya habari nchini Uganda kikiwamo Eyewtnesnews (EWN), kuwa aliahirisha shoo hiyo kwa sababu zake binafsi na si kwa sababu alifukuzwa.

“Sikutokea katika shoo kwa sababu kuna vitu vingi siku nimevielewa na siyo kwa sababu nilifukuzwa,” alisema

Mkongwe huyo wa muziki, alitumia akaunti yake ya twitter kuweka picha ya tiketi ya dege ya daraja la kwanza  kuthibitisha kuwa hakufukuzwa.

“Kama walinifukuza wangenikatia tiketi daraja la kwanza? Alihoji mwanamuziki huyo na kuweka picha ya kikaragosi kikicheka.

Pamoja na utetezi huo, Polisi nchini Uganda waliachia video ya dakika 40 ikimuonyesha msemaji wa Jeshi la Polisi akielezea kwa nini mwanamama huyo alitimuliwa nchini humo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz