Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Yesu' wa Kenya kuhuojiwa kukabiliana na madhehebu yenye utata

Yesu Wa Tongaren 'Yesu' wa Kenya kuhuojiwa kukabiliana na madhehebu yenye utata

Wed, 10 May 2023 Chanzo: Bbc

Mhubiri mwenye utata nchini Kenya ametakiwa kufika polisi kwa mahojiano huku serikali ikikabiliana na kile inachokiita makanisa yenye utata na viongozi wa kidini wenye msimamo mkali.

Eliud Wekesa, almaarufu "Yesu wa Tongaren", kiongozi wa madhehebu ya New Jerusalem, aliitwa Jumanne kuhojiwa kuhusu mafundisho yake ya kidini yanayotiliwa shaka.

Amewaongoza waumini wa kanisa lake kuamini kuwa yeye ni Yesu.

Bw Wekesa ana wanafunzi 12 waliotajwa kwa uzao wa Yakobo wa kibiblia.

Anatarajiwa kufika mbele ya polisi katika kaunti ya magharibi ya Bungoma siku ya Jumatano.

Mhubiri huyo, hata hivyo, anasema hajafanya chochote kibaya ili kuamuru kukamatwa, akiongeza kuwa anaeneza injili pekee, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Haya yanajiri huku wachunguzi wakifukua miili 21 zaidi katika kaunti ya Kilifi pwani, ya Kenya na kufanya jumla ya waliofariki katika mauaji ya Shakahola kufikia 133.

Mchungaji Paul Mackenzie, kiongozi wa Kanisa la Good News International lenye makao yake makuu mjini Kilifi, anasubiri kufikishwa mahakamani, huku kukiwa na shutuma za kuwaamuru wafuasi wake wajiue kwa njaa.

Mamia ya wengine wameripotiwa kupotea.

Rais William Ruto ameunda tume ya uchunguzi kuchunguza vifo vya Shakahola katika kaunti ya Kilifi.

Polisi katika kaunti jirani ya Kwale Jumatatu waliwaokoa watu 200 wakiwemo watoto 50 kutoka msituni katika kisa kinachoshukiwa cha utekaji nyara wa kidini.

Chanzo: Bbc