Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yaliyozungumzwa kwenye mkutano wa Rais Bideni na Uhuru Kenyatta

Biden Uhuru Rais Kenyatta akiwa kwenye mazungumzo na Rais Biden

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Marekani Joe Biden ameitaka Kenya kuchukua hatua muhimu za kulilinda eneo la Afrika Mashariki na kuahidi kuongeza msaada wa chanjo milioni 17 za J&J ili kupambana na Covid-19 kwa Umoja wa Afrika.

At a meeting with President Uhuru Kenyatta at the White House, Mr Biden said Kenya, a traditional ally of Washington, was going to play a significant role, especially now that the region is facing various crises.

Kwenye mkutano na Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya White House, Rais Biden amesema Kenya ni mshirika wa jadi wa Washington, na Marekani itashirikiana nao haswa sasa ambapo Kenya inakabiliana na majanga mbalimbali.

"Mataifa yetu yanashirikiana kwa kujitolea kwa haki na heshima na usawa na nimejitolea kuinua zaidi uhusiano wetu na Kenya na mataifa yote Afrika kwa ujumla, lakini Kenya ni muhimu," Amesema Biden.

Rais Biden ameorodhesha uwazi wa kifedha, amani na usalama kama maeneo muhimi ambayo nchi hiyo inataweka nguvu katika kusaidia Afrika na vile vile mabadiliko ya hali ya hewa kama maeneo muhimu nchi zote mbili zitashirikiana.

Pia aliorodhesha ukuaji wa uchumi, lakini hakuelezea juu ya maswala ya biashara ambayo yalikwama kati ya Kenya na Amerika, kama sehemu ya maeneo ambayo viongozi hao wawili watajadili "kwa kuzingatia kanuni za kuheshimiana na usawa."

Makubaliano ya biashara chini ya mazungumzo ya wakati wa utawala wa Donald Trump yamekwama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live