Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yaibuka Caroline Kangogo alikuwa akishiriki katika wizi wa kimabavu Bonde la Ufa

7521578a5e8bbb11 Yaibuka Caroline Kangogo alikuwa akishiriki katika wizi wa kimabavu Bonde la Ufa

Tue, 13 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Habari zaidi zinadai kuwa Caroline Kangogo alikuwa akishiriki katika sakata kadhaa za uhalifu pamoja na maafisa wenzake ambao sasa wanamlinda Kangogo ni mshukiwa mkuu wa mauaji ya John Ogweno naPeter Ndwiga ambao wanasemekana walikuwa wapenzi wakeLakini makachero wa DCI walisema kuna utata katika mauaji ya wawili hao na madai walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi huenda ni uongo

Uchunguzi na msako wa Caroline Kangogo umechukua mkondo mpya huku makachero wakisema alikuwa sehemu ya kundi linaloshiriki uhalifu katika eneo la Bonde la Ufa.

Habari zaidi zinadai kuwa Kangogo alikuwa akishiriki katika sakata kadhaa za uhalifu pamoja na maafisa wenzake ambao sasa wanamlinda na kumsaidia kuhepa mitego ya polisi.

Duru ilidokezea Daily Nation kuwa, Kangogo ni sehemu ya makundi mawili ya maafisa wa polisi wanaoshiriki wizi wa kimabavu, uporaji na wanalindwa na wanasiasa matajiri na wanabiashara katika eneo la Bonde la Ufa.



Read also

Tharaka Nithi: Watu Watatu Wafariki Dunia Baada ya Kunywa Pombe ya Asali

Kangogo ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji ya Konstebo John Ogweno mjini Nakuru na raia wa kawaida Peter Ndwiga mjini Thika ambao wanasemekana walikuwa wapenzi wake.

Hata hivyo, makachero wa DCI walisema kuna utata katika mauaji ya wawili hao na madai walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi huenda ni uongo.

Huku kundi moja la polisi wahalifu wakitaka kumuua, Kangogo anashukiwa kulindwa na maafisa wa polisi wa kundi analohusiana nalo.

Afisa Mkuu wa DCI katika kaunti ya Nakuru, Anthony Sunguti alisema baadhi ya washukiwa ambao Kangogo alikuwa anawasiliana nao ni maafisa wa ngazi za juu na wahalifu sugu.

Makchero walisema kile kinahitaja kufanywa sasa ni Kangogo kupewa ulinzi mkali dhidi ya maafisa ambao wanata kumuua ili aweze kukamatwa na kupewa nafasi ya kuelezea kilichotokea.

Wahimarisha msakoKatika kupiga jeki msako wao, DCI inatumia idara kadhaa za ujasusi kutoka kwa vitengo vya usalama Kikosi hicho ni ikiwemo polisi, jeshi na wengine kutoka idara za ujasusi.



Read also

Maisha Ilimfinya: Picha ya Mtumishi wa Bwana James Ng'ang'a Kabla ya Kuomoka

Huku akikosa kupatikana kwenye simu, kikosi hicho kitafanya uchunguzi kwenye barabara kuu ikiwemo Nairobi-Nakuru-Eldoret na Nairobi kuelekea Mombasa.

Pia timu hiyo itafanya msako kwenye mahoteli, lojini na maeneo mengine ambazo mshukiwa anadaiwa kujificha.

Ripoti za awali zilidai kwamba simu ya mshukiwa ilionyesha alitembea kaunti sita na wapelelezi wanaamini alikuwa anatumia magari ya umma akiwa amejiicha uso.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke