Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizi wa kura wawaibua wagombea urais Congo, wataka hatua zichukuliwe

Wizi Wa Kura Wawaibua Wagombea Urais Congo, Wataka Hatua Zichukuliwe Wizi wa kura wawaibua wagombea urais Congo, wataka hatua zichukuliwe

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: Voa

Wagombea urais sita huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiwemo wapinzani wakuu wa Rais Felix Tshisekedi Jumanne wameomba hatua za haraka zichukuliwe ili kuzuia wizi wa kura katika uchaguzi mkuu ujao.

Katika taarifa ya pamoja, wagombea hao wameahidi kushirikiana ili kuzuia uchakachuaji wowote wa matokeo na kuitaka tume ya uchaguzi kuchukua hatua kadhaa, ikiwemo kuchapisha orodha ya wapiga kura na ramani ya vituo vya kupigia kura.

Kumekuwa na hali ya mvutano kabla ya uchaguzi wa tarehe 20 Desemba. Washirika wa kimataifa na makundi ya haki za binadamu yamezishtumu mamlaka kukandamiza wapinzani na uhuru wa kujieleza, madai yaliyokanushwa na serikali.

Wagombea wote wa upinzani wameelezea wasiwasi wao juu ya uwezekano wa wizi wa kura na ukosefu wa uwazi.

“Baada ya utata mwingi na ukosefu wa umakini ambao uligubika shughuli zote za kabla ya uchaguzi, ni muhimu siku chache kabla ya kampeni ya uchaguzi, hatua za haraka zichukuliwe kuokoa mchakato wa uchaguzi,” taarifa yao imesema.

Chanzo: Voa