Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizi uliopindukia wafilisi bomba la mafuta kwa siku

Wizi Mafuta Nigeria Wizi uliopindukia wafilisi bomba la mafuta kwa siku

Fri, 29 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uchumi wa Nigeria umepata pigo jingine kubwa baada ya bomba lake la mafuta lenye uwezo wa kusafirisha mapipa 180,000 kwa siku kukumbwa na wizi mkubwa na kulazimika kusimamisha kazi zake tangu mwezi Juni.

Shirika la habari la Bloomberg limenukuu duru moja ya kuaminika ikithibitisha habari hiyo na kusema kuwa, Bomba la Mafuta la Trans-Niger linasubiri tangazo tu la kufungwa kikamilifu kutokana na kufilisiwa na wizi. Kwa mujibu wa Blomberg, bomba hilo lilikuwa linaiingizia serikali ya Nigeria asilimia takriban 15 ya pato lake.

Nigeria ndiye mzalishaji mkubwa zaidi wa mafuta barani Afrika na ni mwanachama wa OPEC wa nchi zinazouza mafuta kwa wingi duniani. Wizi katika mtandao wake wa usafirishaji mafuta umekuwa tatizo sugu katika miaka ya hivi karibuni.

Wataalamu wanasema kuwa, wizi wa mafuta ndiyo sababu ya kushindwa Nigeria kutimiza viwango vinavyotakiwa na OPEC. Serikali ya Nigeria imekuwa ikifanya juhudi mbalimballi za kupambana na wizi wa bidhaa hiyo muhimu lakini imeshindwa na hivi sasa wizi wa mafuta ni katika matatizo sugu yanayoitesa vibaya sekta ya uzalishaji na usafirishaji mafuta nchini Nigeria.

Nigeria inasafirisha karibu mapipa 543,000 ya mafuta kila siku kiwango ambacho ni karibu asilimia 30 chini ya uzalishaji halisi wa bidhaa hiyo nchini humo.

Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA) ilisema mwezi uliopita wa Juni kuwa, wazalishaji mafuta kama Nigeria wameshindwa kutumia fursa ya kufaidika vyema na kupaa bei ya mafuta duniani kutokana na uzembe na udhaifu wao wa kuzalisha viwango vinwavyotakiwa vya mafuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live