Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara yapendekeza ada leseni za magari

4402089eb908040b9050380af46d0f9a Wizara yapendekeza ada leseni za magari

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WIZARA ya Fedha imependekeza ada ya leseni ya kila mwaka ya Sh 200,000 kwa wamiliki wote wa magari kama sehemu ya vyanzo vya mapato katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022.

Waziri wa Fedha, David Bahati amesema hatua hiyo pia inakusudiwa kuimarisha sekta ya uchukuzi kwa kuondoa magari haramu na kukusanya fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara nchini.

Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, wamiliki wa gari watatakiwa kulipa Sh 200,000, wakati wamiliki wa pikipiki watalipa Sh 50,000 kila mwaka.

Waziri huyo alisema hayo mbele ya Kamati ya Fedha ya Bunge na kwamba wanapendekeza ada hiyo ianze kutozwa Julai 1, 2021 baada ya kuingizwa katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali.

Hatua hiyo ina maana ili mtu aweze kuingiza gari barabarani, anatakiwa kuwa na leseni ya barabara badala ya leseni ya udereva na atakayeshindwa kulipia leseni ya barabara anaweza kufungwa jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh milioni 2 au vyote kwa pamoja.

Bahati aliiambia kamati hiyo kuwa ikiwa leseni hiyo itapitishwa, nchi itakuwa na magari yanayostahili barabara na wakati huo huo serikali itapata fedha za kuboresha barabara.

Chanzo: www.habarileo.co.tz