Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya Mambo ya Nje imeanza kutekeleza maagizo ya SADC

SADC WEE Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yaanza kusimamia Maagizo ya SADC

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeagiza kufanyika haraka zoezi la mpango mkakati elekezi wa Jumuiya ya nchi zilizo kusini mwa Afrika - SADC wa mwaka 2020 - 2030 ili kutoa fursa kwa nchi wanachama kuandaa miradi na programu zitakazojumuishwa pamoja kwa lengo la kupewa fedha.

Maagizo haya ya wizara yametolewa kwa wajumbe wa Kamati tendaji wa Wizara mbalimbali wakati wa ufunguzi wa warsha ya kitaifa ya uwekaji gharama katika mpango mkakati elekezi wa maendeleo wa kanda ya SADC – Regional Indictive Strategic Development Plan - RISDP kwa mwaka 2020 – 2030.

Zoezi hilo la uwekaji gharama katika mpango wa utekelezaji wa RISDP ni maelekezo ya baraza la mawaziri wa SADC katika mkutano uliofanyika Agosti 2021 Lilongwe nchini Malawi, ambapo katika mkutano huo nchi wanachama zilielekezwa kutekeleza zoezi la kukamilisha maoni yao katika sekretarieti ya SADC kabla ya Septemba 30 mwaka huu.

Aidha, Wizara imeeleza lengo la mpango huo kuwa ni kuimarisha Ushirikiano katika Kanda kwa ajili ya kuharakisha juhudi za kupunguza umaskini na hatimaye kufikia malengo ya maendeleo ya kiuchumi na yasiyo ya kiuchumi.

Mwisho imeongelea maeneo matano muhimu ambayo mpango huu mpya wa SADC umejikita, maeneo hayo kwanza ni eneo linalohusu Amani, usalama na utawala bora, pili ni maendeleo ya viwanda na ushirikiano wa masoko, tatu ni maendeleo ya miundombinu katika kusaidia ushirikiano wa Kikanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live