Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya Kilimo Yaomba Msamaha Baada ya Akaunti Yake Kumlipua Rais Uhuru

07236d0930dbda5a Wizara ya Kilimo Yaomba Msamaha Baada ya Akaunti Yake Kumlipua Rais Uhuru

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Ujumbe kwenye twitter ulikuwa umemkashifu Rais kwa kuvunja sheria alizoweka Machi 26

- Wanamtandao walisema wizara hiyo ilikuwa imeamua 'huu ni mwaka wa kuambiana ukweli'

- Dakika chache baadaye maafisa wa wizara hiyo waliingia wakihema na kufuta ujumbe huo

Wakenya Alhamisi Aprili 1 walikumbana na ujumbe wa Wizara ya Afya uliowachangamsha wengi.

Kupitia twitter, wizara hiyo ilimzomea Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kwa kufanya mkutano wa hadhara siku chache tu baada ya Rais kupiga marufuku mikutano yote.

Wengi walishangaa ni vipi wizara hiyo ilikuwa imeamua kumzomea mdosi wake hadharani bila woga wa yatakayofuata.

"Ni vipi Rais atapiga marufuku mikutano ya hadhara Machi 26 na kisha kuandaa mkutano wa hadhara Aprili 1?" ujumbe kwenye akaunti hiyo ulishangaa.



Hata hivyo hilo halikukaa kwa muda kwani baadaye wasimamizi wa wizara hiyo waliingia wakihema na kusema lilikuwa ni kosa.

Hayo yalifutwa na kupitia ujumbe mwingine wakasema wahuni walikuwa wameingia kwenye akaunti hiyo na kuanza kujitawala.

Waliomba msamaha na ksuema wamehakikisha kuwa usalama wa akaunti hiyo ni dhabiti ili kuepuka hali kama hiyo siku za usoni.

"Wizara ya Kilimo inaomba msamaha kutoka na ujumbe uliokuwa umetumwa na akaunti hii dakika kama ishirini zilizopita. Ilikuwa imeingiliwa na wahuni kwa muda. Hatua muhimu za kiusalama zimewekwa ili kuhakikisha hilo halijiri tena," ujumbe ulisema.

Jumbe tata zinazidi kutumwa kutoka akaunti za watu mashuhuri au kampuni na kulazimika kuanza kuelezea umma kilichojiri.

Runinga ya Inooro siku chache zilizopita ililazimika kuomba msamaha baada ya kumjibu vibaya mkurugenzi wa bodi ya filamu humu nchini.

"Tunaomba msahama kwa ujumbe uliochapishwa hapa kama jibu kwa Dkt Mutua. Tumetambua ujumbe huo ulitumwa kimakosa na hauonyeshi kwa namna yoyote msimamo wetu kama kituo," msamaha wa Inooro ulisema.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke