Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya Afya Uganda kutoa chanjo kwa bodaboda

Boda Bodaugug Wizara ya Afya Uganda kutoa chanjo kwa bodaboda

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Jiji la Kampala na Wizara ya Afya ya Uganda imeshirikiana na chama cha waendesha bodaboda wa jijini humo kuendesha kampeni kubwa ya kutoa chanjo ya Corona kwa madereva wa bodaboda Jijini humo.

Hatua imekuja mara baada ya Serikali kuanzisha upya zoezi la utoaji wa chanjo hiyo katika maeneo ya Jiji hilo lenye mkusanyiko wa watu wengi.

Nae Mratibu wa zoezi hilo katika jiji humo, Charles Kennedy amesema kuwa Serikali imejipanga kusogeza karibu zoezi hili kwa wananchi wote.

"Katika zoezi la kwanza la kutoa chnajo, tuliweka kipaumbele kuwa watu wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea ndio wapatiwe chanjo, haina maana kuwa watu wenye umri chini ya hapo kuwa hawapo kwenye hatari ya kupata maambukizi ya Corona, kwa wakati ule dozi zilikuwa hazitoshelezi, sasa tunazo za kutosha hivyo niwaombe wananchi wajitokeze kwa wingi kupata chanjo hii" Amesema Bw.Kennedy.

Hata hivyo Chama cha bodaboda katika Jiji hilo, kimeahidi kutoa ushirikiano kwa serikali katika hatua hiyo, na kusisitiza kuwa kitahakikisha madereva wote wanazingatia taratibu zilizowekwa na Wizara ya Afya katika kupambana ugonjwa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live