Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wito watolewa kusaidia wahamiaji waliokwama Afrika

Wahamiaji Woto Msaaada Wito watolewa kusaidia wahamiaji waliokwama Afrika

Fri, 10 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ethiopia, Somalia, Djibouti, Yemen na mashirika 48 ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yameomba msaada wa ufadhili wa dola milioni 84 ili kuwasaidia karibu wahamiaji milioni 1.5 waliokwamba kwenye eneo la Pembe ya Afrika.

Kwenye taarifa yake iliyoitoa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji yaani Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), limebainisha kuwa, hivi sasa kuna zaidi ya wahamiaji 45,000 wamekwama kwenye Ukanda wa Mashariki na wanahitaji msaada wa haraka.

Mohammed Abdiker, mkurugenzi wa shirika la IOM katika eneo la Mashariki na Pembe ya Afrika amesema kuwa, fedha hizo zitatumika kutoa msaada muhimu wa kibinadamu, ahueni ya ulinzi na usaidizi wa maendeleo kwa wahamiaji na jamii zinazowapokea na kuwahudumia wakimbizi hao.

Abdiker pia amesema, msaada huo ni muhimu katika kuokoa maisha ya wahamiaji waliokwama na katika kusudia masuluhisho endelevu ya muda mrefu kwa wahamiaji na jamii zinazowapokea wakati juhudi zikiendelea za kushughulikia utatuzi wa sababu kuu za migogoro inayojitokeza. Makumi ya maelefu ya watu wanahitaji misaada ya dharura Pembe ya Afrika

Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya wanawake na watoto wanaofanya safari hiyo ya kutafuta maeneo salama imeongezeka, ongezeka ambalo ni sawa na asilimia 32 ya wahamiaji kwa mwaka uliopita wa 2022.

Serikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali yametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kukaa pamoja na kuunga mkono mpango huo muhimu wa kuhakikisha wahamiaji wanapata mahitaji muhimu kama vile chakula, malazi na matibabu.

Sababu kuu za watu kuhama maeneo yao ni pamoja na migogoro, athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa na hali mbaya ya kijamii na kiuchumi kwenye maeneo yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live