Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wito wa kujizuia watolewa huku kukiwa na mvutano kati ya vikosi Sudan

Wito Wa Kujizuia Watolewa Huku Kukiwa Na Mvutano Kati Ya Vikosi Sudan Wito wa kujizuia watolewa huku kukiwa na mvutano kati ya vikosi Sudan

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Wajumbe kadhaa wa nchi za Magharibi jana walitoa wito kwa jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kupunguza mvutano baada ya kundi la wanamgambo kuripotiwa kukusanya vikosi vyake katika mji mkuu, Khartoum, na miji mingine, na kuzua hofu ya makabiliano.

Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan (SAF) viliishutumu RSF tarehe 13 Aprili kwa "kuweka vikosi vyake haramu huko Khartoum na miji mingine bila idhini ya uongozi wa jeshi".

Mzozo huo unachangiwa na mzozo unaoendelea kati ya mkuu wa Baraza Kuu tawala, Jenerali Abdel Fatah al-Burhan, na naibu wake na kamanda wa RSF Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo.

Magari mapya ya kivita ya RSF yanaripotiwa kuingia Khartoum Alhamisi, siku moja baada ya jeshi la wanamgambo kutuma wapiganaji katika mji wa kaskazini wa Merowe, ambako SAF ina kambi ya anga.

Inasemekana kuwa jeshi lilikuwa limewapa wanajeshi wa RSF huko Merowe "masaa 24 kuondoka, la sivyo wangelazimika kufanya hivyo".

RSF inasema uwepo wake katika mji unakuja "ndani ya mfumo wa kutekeleza majukumu yake" kote Sudan.

Katika taarifa, wajumbe wa Ufaransa, Ujerumani, Norway, Uingereza, Marekani na Umoja wa Ulaya walionyesha wasiwasi wao juu ya hali hiyo na kulitaka jeshi na RSF "kuchukua hatua za kupunguza mvutano".

Dagalo amefanya mazungumzo ya simu na baadhi ya wajumbe, "akiwaeleza hali ya Sudan", kulingana na shirika la habari la serikali la Suna.

Mvutano huo umesababisha kucheleweshwa kwa kuundwa kwa serikali inayoongozwa na raia huku kukiwa na kutoelewana juu ya kuunganishwa kwa RSF katika jeshi.

Chanzo: Bbc