Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wimbi la wakimbizi wa DRC laongeza kasi ya COVID-19 Uganda

Wakimbizi DRC DRC Wimbi la wakimbizi wa DRC laongeza kasi ya COVID-19 Uganda

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya wakimbizi 62,000 wa Kongo wameingia Uganda tangu Januari na idadi hiyo imeongezeka katika wiki chache zilizopita kufuatia mapigano mapya kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23.

Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Uganda, wengi wa wakimbizi hao hawajachanjwa dhidi ya Covid-19.

Itifaki ya shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu kuhudumia wakimbizi ni kwamba wakimbizi wanapaswa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kuhusu magonjwa kadhaa, ikiwa ni pamoja na Covid-19, katika vituo vya kuwapokea karibu na mpaka.

Hata hivyo imekuwa vigumu kwa serikali ya Uganda kudhibiti mienendo ya wale wanaotoka DRC, huku wengi wao wakikataa kwenda kwenye vituo rasmi vya mapokezi kwa ajili ya kuchunguzwa, wakiamua kubaki mpakani wakisubiri mapigano kupungua.

Msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Uganda Irene Nakasiita ameliambia gazeti la The East African kuwa, "Kwa hofu ya kushughulikiwa kama wakimbizi, wengi waliweka makazi ya muda katika mpaka ambapo wanachanganyikana na jamii,"

Kufikia Alhamisi, data rasmi ilionyesha kuwa Uganda ilikuwa imetoa dozi milioni 21.7 za chanjo ya Covid-19, kati ya hizo milioni 16 zilikuwa dozi moja na dozi milioni 10 mara mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live