Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

William Ruto ataka kesi ya kupinga ushindi wake ifutwe

IMG 20220 Rutoo William Ruto ataka kesi ya kupinga ushindi wake ifutwe

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

William Ruto amewasilisha majibu yake kwenye kesi iliyowasilishwa na Raila Odinga wa Azimio katika Mahakama ya Juu, kupinga ushindi wake kwenye uchaguzi wa Agosti 9, 2022.

Kwenye majibu hayo ya kurasa 256, Ruto anaitaka Mahakama hiyo kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Raila kwa sababu anataka handshake ili akabidhiwe mgao wa serikali.

Ruto ameongeza kusema kwamba Raila ana rekodi za kupinga kila matokeo ya uchaguzi mkuu, kiasi cha kulazimisha maelewano yatakayomwezesha kupata sehemu ya serikali.

Rais mteule William Ruto amewasilisha majibu yake kwenye kesi iliyowasilishwa na Raila Odinga wa Azimio katika Mahakama ya Juu, kupinga ushindi wake kwenye uchaguzi wa Agosti 9.

Naibu Rais William Ruto. Picha: UGC. Kwenye majibu hayo ya kurasa 256, Ruto anaitaka Mahakama hiyo kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Raila kwa sababu anataka handshake ili akabidhiwe mgao wa serikali.

Ruto ameongeza kusema kwamba Raila ana rekodi za kupinga kila matokeo ya uchaguzi mkuu, kiasi cha kulazimisha maelewano yatakayomwezesha kupata sehemu ya serikali.

Azimo Yataka Kesi Zilizowasilishwa na Moses Kuria, Reuben Kigame Kuondolewa Katika Mahakama ya Juu Ruto alitoa mfano wa serikali ya nusu mkate iliyoundwa baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007, enzi za Mwai Kibaki na ya punde mwaka wa 2017 waliposalimiana na Rais anayeondoka Uhuru Kenyatta.

“Hulka ya kwanza inayojulikana ni kwamba kwa kipindi cha miaka 30 amekuwa akipinga matokeo ya uchaguzi mkuu na kukimbia mahakamani baada ya uchaguzi wa urais kutangazwa.

Hatua yake imeonekana ni juhudi za kumlazimisha mshindi wa urais kumgawanyia mamlaka kupitia njia zisizotambulika kwa mujibu wa katiba almaarufu handshake,” Ruto alisema siku ya Ijumaa, kwenye majibu ya kesi hiyo kupitia mawakili wake.

Kwenye kesi aliyowasilisha katika mahakama hiyo, Raila anataka ushindi wa Ruto ubatilishwe, kwa kusema kwamba hakushinda kihalali kwa kuwa Tume ya IEBC, ilisimamia uchaguzi uliogubikwa na ulaghai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live