Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

William Ruto afunguka baada ya kuzuiwa kufanya ziara Uganda

3e8b514e052050d0 Naibu Rais William Ruto

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

William Ruto alisema kuwa hatua ya kuzuia safari yake ya Uganda ilikusudiwa kumsukuma kuzozana na watu wengine serikalini Ruto alisema urafiki wake na Museveni umeonekana kuwanyima usingizi watu wengineAlibainisha kwa kipindi amekuwa naibu rais hajawahi hitajika kuomba rhusa kwa yeyote kwenda nje ya nchiNaibu Rais William Ruto amesema hajawahi hitajika kuomba ruhusa kutoka kwa mtu yeyote kusafiri nje ya nchi kwa miaka tisa ambayo amekuwa katika cheo hicho.

Hisia za Ruto zinajiri kufuatia agizo la hivi karibuni lililomzuia kusafiri kwenda Uganda baada ya maafisa wa uhamiaji kukataa kumpa idhini katika uwanja wa ndege wa Wilson.

Akiongea Inooro FM Jumatano, Agosti 4, naibu rais alisema hatua ya kuzuia safari yake ilikusudiwa kumsukuma kuzozana na watu wengine serikalini.

"Nimekuwa naibu rais kwa miaka tisa na nimesafiri kwenda nchi nyingi kwa sababu za kikazi na za kibinafsi. Hamna siku hata moja nimetakiwa kumuomba yeyote ruhusa hadi hapo Jumatatu.



Read also

Magazeti Jumanne, Agosti 3: Sababu ya Ruto Kuzuiwa Kutangatanga Uganda

"Je! Ni sheria ipi ambayo imeanza hivi karibuni? ilikusudiwa ili kusababisha mzozo lakini nimemuwachia Mungu," alielezea.

DP alibaini kuwa Museveni ni rafiki wa karibu wa Rais Uhuru Kenyatta na wanasiasa wengine wengi nchini Kenya akiongeza kuwa ilionekana kuwa shida baada ya yeye (Ruto) kuunda urafiki na rais huyo.

"Sina haki ya kuwa na marafiki?" aliuliza.

Alisema pia ni makosa kumtaja Harun Aydin raia wa Uturuki kama gaidi kutokana na uhusiano wake na DP lakini alikuwa mwekezaji mwaminifu.

Jamaa huyo pia alipaswa kusafiri na DP kwenda Entebbe, Uganda wakati safari yao ilifutiliwa mbali.

Kama ilivyoripotiwa hapo awali na TUKO.co.ke, Ruto alizuiwa kwenda katika nchi hiyo jirani ya Kenya kwa madai kwamba alikuwa hajafutuata idhini kama mfanyakazi wa umma

Kulingana na ofisi ya DP, ndege iliyofaa kumbeba ilikuwa tayari na agizo na kumzuia kuondoka lilikuja baada yake kusubiri kwa saa kadhaa katika uwanja wa Wilson.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Read also

Binti Akamatwa Baada ya Dume Aliyekuwa Akionja Tunda Katika Lojing'i Kuzima

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke