Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wiki chache za mafuriko ya maafa katika Pembe ya Afrika

Mafuriko 145620 Wiki chache za mafuriko ya maafa katika Pembe ya Afrika

Sun, 19 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mafuriko makubwa katika eneo la Pembe ya Afrika yamesababisha zaidi ya watu mia moja kupoteza maisha na mamia kwa maelfu ya wengine kuhama makazi yao.

Ripoti ya shirika la "Save the Children", inasema takriban watu 111, wakiwemo watoto 16, wamepoteza maisha yao katika mafuriko ya mvua kubwa katika kipindi cha wiki za karibuni katika Pembe ya Afrika, na Maelfu 700 ya watu kuhama makazi yao. Hali ya hewa ya El Nino imeongeza mvua katika eneo hilo, na kuathiri hasa nchi za Somalia, Ethiopia na Kenya.

Eneo la Pembe ya Afrika ni mojawapo ya maeneo yaliyoathirika zaidi na mabadiliko hayo ya hali ya hewa, na matukio mengi ya kusikitisha yanaendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.

Mafuriko Pembe ya Afrika Tangu mwishoni mwa 2020, Somalia, pamoja na sehemu za Ethiopia na Kenya, zimeathirika kutokana na ukame mkubwa ambao ulikuwa haujawahi kushuhudiwa katika eneo hilo katika miaka 40.

Hali ya El Nino, ambayo kwa kawaida hupelekea kuongezeka joto na ukame katika baadhi ya maeneo ya dunia pamoja na mvua kubwa katika maeneo mengine, inatarajiwa kuendelea hadi mwezi Aprili.

Hali hii ya hewa tayari imesababisha uharibifu mkubwa Afrika Mashariki. Kuanzia Oktoba 1997 hadi Januari 1998, mafuriko makubwa, yaliyosababishwa na mvua kubwa za El Nino yalipelekea zaidi ya watu elfu 6 kupoteza maisha katika eneo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live