Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wezi wachimba ukuta wa choo cha pasta na kuiba vyombo vya KSh1M Mombasa

6c2988e28295318b Wezi wachimba ukuta wa choo cha pasta na kuiba vyombo vya KSh1M Mombasa

Mon, 17 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Wezi hao walichimba shimo kupitia kwenye ukuta wa choo cha pasta na kuingia kwenye stoo ya kanisa hilo

- Wezi hao walitoweka na spika, vipaza sauti, swichi za elektroniki, viti vya plastiki na vifaa vingine vya kielektroniki.

- Pasta wa kanisa hilo alishangazwa na namna wezi hao walifaulu kuchimba shimo usiku wakati polisi walikuwa nje wakitekeleza amri ya kafyu

Ibada katika Kanisa la Holy Trinity Africa, kaunti ya Mombasa ilisambaratika Jumapili, Mei 16, baada ya waumini kupata mali yenye thamani ya KSh1 milioni imeibwa usiku.

Ripoti zinadai kuwa wezi walichimba shimo kupitia kwenye ukuta wa choo cha pasta na kuingia kwenye stoo ya kanisa hilo.

Kulingana na pasta wa kanisa hilo Joshua Owiti, wezi hao walitoweka na spika, vipaza sauti, swichi za elektroniki, viti vya plastiki na vifaa vingine vya kielektroniki.

Owiti alishangazwa na namna wezi hao walifaulu kuchimba shimo usiku wakati polisi walikuwa nje wakitekeleza amri ya kafyu.

"Tunaomba polisi kufanya uchunguzi na kuwakamata wahalifu hao. Sasa tumesambaratika kama kanisa sasa tunahitaji msaada kununua vifaa vingine vipya kwa sababu ni bei ghali," alisema.

Simon Ayieko ambaye hudumisha usafi katika kanisa hilo ndiye alikuwa wa kwanza kupiga ripoti baada ya kuwasili kanisani mapema asubuhi na kupata vyombo vimeibwa.

"Punde nilipopiga ripoti kwa uongozi wa kanisa, walichukuwa hatua za haraka na kuripoti kwa kituo cha polisi cha Makupa,"

"Polisi waliandamna nasi wakawahoji majirani na tunatumai watawakamata wezi hao," Ayieko alisema.

Katika taarifa sawia na hiyo ya kisa cha wizi kanisani, watu wasiojulikana waliripotiwa kuiba kengele ya kanisa la Virgin Mary Orthodox lililoko eneo la Limuru kaunti ya Kiambu.

Kulingana na katibu wa kanisa hilo James Warari ambaye alizungumza na TUKO.co.ke, genge la wezi lilivamia kanisa hilo Alhamisi, Aprili 22 na kuiba kengele hiyo ambayo inasemekana kuwa na uzito wa kilogramu 500.

Warari alisema kengele hiyo ilikuwa imetengenezwa na shaba na ilikuwa ikitumiwa kuwakumbusha waumini saa za kuomba na pia kupanga ratiba ya kanisa hiyo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke