Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenye kadi zilizoharibika waruhusiwa kupiga kura DRC

Kuraaa.png Wenye kadi zilizoharibika waruhusiwa kupiga kura DRC

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC (CENI) Denis Kadima amesema kuwa wapiga kura wote waliosajiliwa rasmi wataruhusiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika wiki ijayo hata ikiwa kadi za kupigia kura zimeharabika

Kuali hiyo ya CENI imeungwa mkono na uamuzi wa Mahakama ya Katiba ambayo imeyakataa madai yote ya kuahirisha uchaguzi yaliyotolewa na wagombea Urais wa upinzani

Mahakama imesema kuwa madai yao hayana msingi na mchakato wa uchaguzi utaendelea kama ilivyopangwa

Kumękuwa na wasi wasi kuwa idadi kubwa ya wapiga kura huenda wasishiriki uchaguzi huo baada ya maelezo kwenye kadi zao kufutika hiyo kauli ya Tume inaweza kuleta matumaini kwa wapiga kura

Tume ya uchaguzi imekuwa ikiendesha shughuli ya kuwapa wapiga kura wałiosajiliwa kadi mpya ikiwa kadi żao zimeharibika łakini zoezi lenyewe limekuwa likienda pole pole kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza ili kupata kadi mpya

Kadima ameongeza kuwa hadi sasa hawajafanikiwa kupata ndege za kutosha kusafirisha vifaa vitakavyotumika wakati wa uchaguzii hadi maeneo yote

Siku mbili zilizopita CENI iliiandikia serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa kuipa misaada ya ndege ili kufanikisha shughuli ya kusafirisha vifaa vya kupigia kura

Chanzo: www.tanzaniaweb.live