Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wengi wakamatwa Nigeria kwa madai ya harusi ya wapenzi wa jinsi moja

Wengi Wakamatwa Nigeria Kwa Madai Ya Harusi Ya Wapenzi Wa Jinsi Moja Wengi wakamatwa Nigeria kwa madai ya harusi ya wapenzi wa jinsi moja

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Vikosi vya usalama nchini Nigeria vimewakamata zaidi ya watu 70 kwa madai kwamba waliandaa karamu yawapenzi wa jinsi iliyojumuisha sherehe ya harusi kati ya wanaume wawili.

watu hao walimamatwa Jumamosi katika mji wa Gombe, jimbo lenye Waislamu wengi kaskazini mwa Nigeria, lakinitaarifa hiyo ilithibitishwa Jumatatu.

"Tuliwakamata washukiwa 76 wa jinsi moja wakifanya karamu ya kuzaliwa iliyoandaliwa na mmoja wao, ambaye alipaswa kumuoa bibi harusi wake wa kiume kwenye hafla hiyo," Buhari Saad, msemaji wa Kikosi cha Usalama na Ulinzi wa Raia wa Nigeria, aliliambia shirika la habari la AFP.

Washukiwa hao ni pamoja na wanaume 59 na wanawake 17, huku 21 kati ya wanaume "wakikiri kwa utashi wao kuwa ni wapenzi wa jinsi moja," aliongeza.

Ni msako wa hivi punde zaidi dhidi ya wapenzi wa jinsi moja nchini Nigeria, ambapo sheria ya mwaka 2014 ilikataza uhusiano wa watu wa jinsia moja na ndoa.

Sheria hiyo ilianzisha kifungo cha hadi miaka 14 jela kwa wale wanaopatikana na hatia kwa makosa hayo.

Mwezi Agosti, vikosi vya usalama viliwakamata watu 67 kwa madai ya kuhudhuria harusi ya wapenzi wa jinsi moja katika jimbo la Delta kusini, lakini mahakama iliwaachilia kwa dhamana.

Chanzo: Bbc