Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa zamani wa Utalii Najib Balala akamatwa kwa tuhuma za ufisadi

Najib Balala.jpeg Waziri wa zamani wa Utalii Najib Balala akamatwa kwa tuhuma za ufisadi

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Maafisa wa upelelezi wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi(EACC) nchini Kenya wamemkamata Waziri wa zamani wa Utalii Najib Balala, vyomba ya habari nchini vinaripoti.

Hatua hiyo inafuatia madai kwamba Hazina ya Utalii ililipa kwa ulaghai shilingi bilioni 8.5 ili kuanzisha tawi la Pwani la Chuo cha Utalii nchini Kenya (baadaye kilipewa jina la Ronald Ngala Utalii College) wakati huo akiwa waziri.

Balala alikamatwa pamoja na watu wengine watatu akiwemo Leah Adda Gwiyo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii, na Joseph Odero wa Wahandisi wa kampuni ya West Consult Engineers..

EACC ilifanya uchunguzi kuhusiana na malipo hayo na kuwasilisha ripoti ya uchunguzi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ambaye alikubaliana na mapendekezo ya kukamatwa na kuwafungulia mashtaka watu 16.

Washukiwa hao wanakabiliwa na makosa 10 ya ufisadi na uhalifu wa kiuchumi, ikiwa ni pamoja na ulaghai wa ununuzi na ufujaji wa Shilingi bilioni 8.5 za umma, EACC ilisema

Msemaji wa Tume hiyo Eric Ngumbi aliyenukuliwa na vyombo vya habari alisema Bw Balala atasafirishwa hadi Mombasa kutoka Nairobi na baadaye kupelekwa katika mahakama ya Malindi pwani ya Kenya.

Maafisa wa upelelezi kwa sasa wanawasak washukiwa zaidi wa kesi hiyo.

Chanzo: Bbc