Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa zamani wa Gambia atupwa jela miaka 20

Ousman Sonko 1 1 Aliyewahi kuwa Waziri wa Ulinzi nchini Gambia, Ousman Sonko

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama nchini Uswisi imemuhukumu kifungo cha miaka 20 Gerezani aliyewahi kuwa Waziri wa Ulinzi nchini Gambia, Ousman Sonko baada ya kukutwa na hatia ya ukikuwaji wa haki za binadamu.

Bw.Sonko mwenye umri wa miaka 55 amekutwa na hatia ya kutenda makosa hayo kati ya mwaka wa 2000 na 2016 wakati wa utawala Yahya Jammeh.

Taarifa ya hukumu yake ilitangazwa na wakala wa Mahakama ambapo Sonko ana muda wa kukata rufaa kuhusu hukumu hiyo.

Sonko ambaye alikamatwa mwaka wa 2017 akiwa anakimbilia uhamishoni nchini Uswisi anashutumiwa pia katika ubakaji wa wanawake,mauaji,unyanyasaji na kuhatarisha usalama wa nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live