Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa zamani wa Gambia akabiliwa na mashtaka ya kuamuru mateso

Waziri Wa Zamani Wa Gambia Akabiliwa Na Mashtaka Ya Kuamuru Mateso Waziri wa zamani wa Gambia akabiliwa na mashtaka ya kuamuru mateso

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Gambia atafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu nchini Uswizi akituhumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu.

Ousman Sonko anakabiliwa na orodha ndefu ya mashtaka, ikiwa ni pamoja na kushiriki au kuamuru mauaji, mateso na ubakaji wa wapinzani wa kisiasa.

Sonko amekana mashtaka yote, shirika la habari la AFP linaripoti, likimnukuu wakili wake Philippe Currat.

Alikimbilia Uswizi mwaka 2016, muda mfupi kabla ya utawala kandamizi wa rais wa Gambia Yahya Jammeh kupoteza mamlaka, lakini alikamatwa baada ya mashirika yasiyo ya kiserikali kuwasilisha mamlaka ya Uswizi na ushahidi wa kuhusika kwake katika ukiukaji wa haki za binadamu.

Tisa kati ya waathiriwa wake watakuwa mahakamani kutoa ushahidi.

Ndiye afisa wa ngazi ya juu kabisa serikalini kuwahi kushitakiwa kwa njia hii barani Ulaya.

Uswizi inaendesha kesi hiyo chini ya mkuu wa mamlaka ya ulimwengu, ambayo inaruhusu nchi kushtaki watu katika eneo lao, ingawa uhalifu unaodaiwa ulitekelezwa mahali pengine.

Chanzo: Bbc