Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa zamani DRC Ponyo ajiondoa kinyanganyiro cha urais

Waziri Wa Zamani DRC Ponyo Ajiondoa Kinyanganyiro Cha Urais Waziri wa zamani DRC Ponyo ajiondoa kinyanganyiro cha urais

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Waziri mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Augustin Matata Ponyo amejiondoa kutoka kinyanganyiro cha kuwania urais na badala yake kutangaza anamuunga mkono Moise Katumbi, gavana wa zamani wa jimbo la Katanga.

Hayo yanawadia wakati kipindi rasmi cha kampeini kikianza jana Jumapili nchini Congo kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa tarehe 20 mwezi ujao Desemba ambapo Rais Felix Tshisekedi anawania muhula wa pili madarakani.

Bwana Tshisekedi alikuwa miongoni mwa wagombea waliozindua kampeini zao jana mjini Kinshasa. Ameahidi kuhakikisha taifa hilo lina chakula cha kutosha.

"Lengo letu ni kuanza kuzalisha humu nchini kwasababu kilimo chetu kina uwezo wa kulisha raia wa Congo wote na hatuhitaji kununu unga wa mahindi, muhogo au mchele kutoka nje. Tunanunua mpaka mbegu kutoka nje na hilo sasa litakwisha, tutaanza kutengeza mbegu zetu. Mkiniamini mtafurahi, niaminini tena na mtaona tutalijenga taifa letu pamoja.")

Wengine wanaowania Urais ni Martin Fayulu na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Dkt Dennis Mukwege miongoni mwa wengine.

Chanzo: Bbc