Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa tatu ajiuzulu Rwanda

95965 Rwanda+pic Waziri wa tatu ajiuzulu Rwanda

Mon, 17 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigali, Rwanda. Mawaziri watatu nchini Rwanda wamejiuzulu ndani ya wiki moja.

Dk Diane Gashumba aliyekuwa Waziri wa Afya alitangaza kujiuzulu wadhifa wake Ijumaa iliyopita.

Taarifa ya ofisi ya waziri mkuu ilisema kuwa Dk Diane aliwasilisha barua ya kujiuzulu mapema asubuhi.

Katika ujumbe wake wa Twitter, ofisi hiyo ilisema kujiuzulu kwa waziri huyo kunatokana na makosa ya kawaida na mapungufu katika uongozi wake.

Hata hivyo, taarifa hiyo haikutoa maelezo zaidi kuhusu mapungufu hayo.

Dk Diane ambaye kazi yake inahusisha pia kudhibiti kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola kuingia nchini Rwanda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), amekuwa waziri wa afya kwa miaka minne tangu alipoteuliwa na Rais Paul Kagame Oktoba 2016.

Pia Soma

Advertisement
Kujiuzulu kwa Dk Diane kumekuja siku mbili baada ya mawaziri wengine wawili kutangaza kuachia nafasi zao ndani ya wiki moja.

Waziri mwingine ni Evode Uwizeyima ambaye alikuwa akisimamia masuala sheria.

Uwizeyima alitangaza kujiuzulu baada ya kukumbwa na kashfa ya kumpiga mlinzi.

Mwingine ni Isaac Munyakazi aliyetangaza kujiuzulu Jumatano iliyopita.

Munyakazi alikuwa waziri anayesimamia sekta ya elimu nchini humo.

Hata hivyo, haikuweka bayana sababu hasa ya waziri huyo kuchukua uamuzi huo.

Chanzo: mwananchi.co.tz