Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov anafanya ziara ya kwanza nje ya nchi tangu Urusi ilipoivamia Ukraine - ikiwa ni sehemu ya ziara mpya ya kidiplomasia katika eneo hilo.
Ziara ya Waziri wa Urusi Sergie Lavrov Kusini mwa Afrika imepangwa kikamilifu.
Sio siri kwamba Urusi imetengwa na idadi ya nchi zenye nguvu za Magharibi - tangu uvamizi wake wa Ukraine karibu mwaka mmoja uliopita - huku nchi nyingine zikitafuta namna ya kupunguza kufanya biashara na Urusi - kama ishara ya maandamano.
Lakini kwa Afrika Kusini, mambo si hivyo.
Nchi hizo mbili zina uhusiano wa kihistoria kuanzia vita vya Afrika Kusini vya kukomesha ubaguzi wa rangi...na katika miaka ya hivi karibuni - uhusiano wa karibu wa kibiashara kupitia kambi ya Brics ya mataifa yanayoibukia kiuchumi, ambayo nchi zote mbili ni wanachama.
Licha ya shinikizo fulani la kuunga mkono uvamizi wa Urusi, Afrika Kusini imebakia kutoegemea upande wowote.
Ingawa Lavrov hakupendezwa na hali hiyo - shirika la kiraia la Chama cha Kiukreni cha Afrika Kusini kimesema kitafanya maandamano katika mji mkuu wa Preotria ambako mawaziri wanakutana - ili kuonesha kutofurahishwa kwao na uhusiano mzuri wa nchi hizo mbili.