Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani awasili Rwanda

RWANDA ONEEE Waziri wa mambo ya nje wa Marekani awasili Rwanda

Thu, 11 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amewasili nchini Rwanda katika ziara iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mazungumzo kuhusu madai ya nchi hiyo kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaoendesha harakati zao katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Bw Blinken pia anatarajiwa kuishinikiza Kigali kumwachilia Paul Rusesabagina, mhusika wa filamu iliyoteuliwa na Oscar Hotel Rwanda, ambaye serikali ya Marekani inasema "amezuiliwa kimakosa nchini Rwanda".

Rusesabagina alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa ugaidi na mahakama ya Rwanda mwaka jana katika kile ambacho wafuasi wake walikiita kesi ya uongo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inasema mjini Kigali, Bw Blinken "atakutana na viongozi wa Rwanda na wanachama wa mashirika ya kiraia kuhusu masuala mbalimbali muhimu".

Akijibu kwenye ukurasa wa Twitter kuhusu shinikizo linalotarajiwa na Marekani, Rais Kagame alisema: "Hakuna wasiwasi...kuna mambo ambayo hayafanyiki hivyo hapa!!"

Bw Blinken aliwasili Kigali Jumatano usiku kutoka Kinshasa ambako mamlaka iliiomba Marekani kuiwekea vikwazo Rwanda kwa "kuwaunga mkono waasi wa M23" ambao sasa wanadhibiti sehemu za jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa DR Congo.

Rwanda imekana kuunga mkono kundi la M23, na waasi hao wanakanusha madai kwamba walipigana pamoja na wanajeshi wa Rwanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live