Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa kwanza kuzungumzia ubakaji wa Tigray Ethiopia ajizulu

Ethio Pic Waziri wa kwanza kuzungumzia ubakaji wa Tigray Ethiopia ajizulu

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa masuala ya Wanawake nchini Ethiopia ambaye amekuwa Afisa wa kwanza kuzungumza kuhusu vitendo vya ubakaji wa wanawake vilivyofanyika wakati wa vita ya Tigray, ametangaza kujihuzulu nafasi hiyo pasipo kutaja sababu dhahiri kuhusu maamuzi hayo.

Waziri huyo, Filsan Abdullahi Ahmed, ametoa taarifa hiyo kupitia mtandao wa Twitter huku akisema kuwa hayupo tayari kufanya kazi nje na maadili na imani aliyojiwekea kwani kufanya hivyo kwake ni kujivunjia heshima.

"Sipo tayari kufanya jambo lolote lile linayokinzana na maadili yangu ya kazi, kufanya hivyo ni kujisaliti, na kujivunjia heshima, kukana imani yangu pamoja na kuvunja imani ya wananchi juu yangu"

"Kwasababu binafsi zinazotokana na dhamiri yangu mwenyewe, kwa masikitiko makubwa nimewasilisha barua ya kujiuzulu nafasi hii" ameandika Waziri huyo kupitia mtandao wa Twitter.

Mnamo mwezi Februari, 2021 Filsan alitoa taarifa kuhusu vitendo vya ubakaji vilivyofanyika wakati ya vita hiyo baina ya waasi wa Tigray na Seriklai , alianzisha kikosi kazi cha kufatilia suala hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live