Waziri wa Ulinzi nchini Uganda, Maj Gen Muhwezi ameripotiwa kumilika hisa katika kampuni mbili zilizopo nchini Uingereza katika visiwa vya BVI na Cyprus kati ya mwaka 2015 na 2018.
licha ya Waziri huyo kukataa madai hayo, bado jina lake limeonekana katika nyaraka za za kampuni hizo zilizovuja zikimuonesha kuwa mmoja wa wamiliki watatu wa kampuni hizi mbili.
Taasisi ya Waandishi wa Habari za Uchunguzi (ICIJ), yenye maskani yake Washington DC, Marekani, Septemba 3, mwaka huu, ilitoa ripoti yenye kuwaonesha wanasiasa 336 duniani, wenye kampuni zinazofanya kazi kwa kukwepa kodi, vilevile wanaojipatia fedha kifisadi, hata hivyo baadhi ya waliotajwa wamekana.
Ripoti hiyo imeonesha kuwa Kiongozi huyo aliwekeza katika Kampuni hizo tarehe 3 Februari, 2015.
"Hii ni kuthibitisha kuwa ndugu Katugugu Jim Muhwezi anamiliki jumla ya hisa 1,333 katika kampuni hii tajwa hapo juu, kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa pamoja Nakala za Kampuni" imesomeka Nyaraka hiyo iliyovuja.
Mpaka sasa hakuna hatua za kisheria zilizochukuliwa na vyomba vya usalama nchini humo kufuatia madai haya kwa kiongozi huyo.