Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa Uingereza ajiuzulu kutokana na mswada wa wahamiaji wa Rwanda

Waziri Wa Uingereza Ajiuzulu Kutokana Na Mswada Wa Wahamiaji Wa Rwanda Waziri wa Uingereza ajiuzulu kutokana na mswada wa wahamiaji wa Rwanda

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Robert Jenrick amejiuzulu kama waziri wa uhamiajinchini Uingereza, akisema sheria ya dharura ya serikali ya Rwanda "haijitoshelezi".

Alisema "ulinzi madhubuti" ulihitajika ili kumaliza "mfululizo wa changamoto za kisheria ambazo zinaweza kudhoofisha mpango huo".

Serikali ilisema mswada huo, uliozinduliwa mapema, uliweka wazi katika sheria za Uingereza, Rwanda ilikuwa nchi salama kwa wanaotafuta hifadhi.

Lakini hauelezei kile ambacho baadhi ya wabunge wa chama cha Kihafidhina cha Conservative wanachodai.

Katika barua yake ya kujiuzulu kwa Rishi Sunak, Bw Jenrick alisema waziri mkuu "ameelekea kwenye msimamo wangu" kuhusu sheria ya dharura.

"Hata hivyo, siwezi kuchukua sheria inayopendekezwa kwa sasa kupitia Bunge kwani siamini kwamba inatupa fursa nzuri zaidi ya kufaulu."

Bw Jenrick aliongeza kuwa mswada huo ni "ushindi wa matumaini dhidi ya uzoefu".

Kujibu, waziri mkuu alielezea kujiuzulu kwa Bw Jenrick kama "kuvunja moyo" na "kutokana na kutoelewa hali hiyo".

"Ikiwa tungeondoa mahakama kabisa, tungevunja mpango mzima," Bw Sunak alisema.

"Serikali ya Rwanda imekuwa wazi kwamba haitakubali Uingereza kuegemeza mpango huu upande wa sheria ambayo inaweza kuchukuliwa kuwa inakiuka wajibu wetu wa sheria za kimataifa."

Chanzo: Bbc