Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa Masuala ya kigeni apiga madai serikali inatumia nguvu kupitia kiasi

Waziri Wa Masuala Ya Kigeni Apiga Madai Serikali Inatumia Nguvu Kupitia Kiasi Waziri wa Masuala ya kigeni apiga madai serikali inatumia nguvu kupitia kiasi

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Dkt. Alfred Mutua amepinga madai ya Umoja wa Mataifa kuwa mamlaka za serikali zinatumia nguvu kupita kiasi kuzima maandamano ya kuipinga serikali kote nchini.

Haya yanajiri baada ya msemaji wa Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, Jeremy Laurence, kusema kuwa shirika hilo "limesikitishwa sana na ghasia zilizoenea, na madai ya matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima , ikiwa ni pamoja na matumizi ya silaha za moto, na polisi wakati wa maandamano yanayoongozwa na Muungano wa Azimio la Umoja."

Akizungumza leo Bw Mutua aliitaja kauli hiyo ya Umoja wa Mataifa kama propaganda zisizo sahihi na za kupotosha zinazolenga kuwanyima Wakenya uhuru wao wa kidemokrasia.

Chanzo: Bbc