Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa Mambo ya nje Marekani afanya mazungumzo viongozi wa Sudan

Waziri Wa Mambo Ya Nje Marekani Afanya Mazungumzo Viongozi Wa Sudan Waziri wa Mambo ya nje Marekani afanya mazungumzo viongozi wa Sudan

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken amezungumza na kamanda wa vikosi vya wanajeshi wa Sudan Abdel Fattah al Burhan na kamanda wa vikosi vya wanamgambo wa RSF Mohammed Hamdan Dagalo.

Blinken aliandika kwenye tweeter kwamba alisisitiza haja ya dharura ya kusitisha mapigano na umuhimu wa kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wa kidiplomasia na wafanyakazi wa misaada.

RSF ilikubali kupigiwa simu na Blinken kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii lakini haijatoa ahadi ya kusitisha mapigano.

Usitishaji vita wa pili wa saa 3 jana usiku haukufua dafu, huku pande zote zikilaumiana kwa uvunjaji huo.

Mwanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya alivamiwa katika makazi yake, huku Umoja wa Mataifa ukisema mashirika yake, maghala na nyumba za wageni zimepigwa risasi na kuporwa.

Baadhi ya nyumba za raia pia zimevunjwa na wakazi walivamiwa, lakini RSF inakanusha kuhusika.

Takriban watu 200 wameuawa tangu mapigano kati ya RSF na jeshi yalipozuka siku ya Jumamosi huku wakiwa hawakubaliani juu ya mustakabali wa Sudan na kuunganishwa kwa RSF katika jeshi la taifa.

Chanzo: Bbc