Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri mkuu mstaafu wa Sudan afariki kwa corona

Mtanzanianews 127302093 1755496684625863 4110498121285475209 N 660x400 Waziri mkuu mstaafu wa Sudan afariki kwa corona

Thu, 26 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Waziri mkuu wa zamani wa Sudan, Sadiq al-Mahdi amefariki dunia kutokana na virusi vya corona, mwanasiasa huyo amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mahdi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 84, ndiye waziri mkuu wa mwisho wa Sudan kuchaguliwa kidemokrasia kabla ya kuondolewa madarakani mwaka 1989 kwa mapinduzi ya kijeshi yaliyomuingiza mamlakani rais wa zamani Omar al-Bashir.

Chama chake cha Umma chenye siasa za wastani, kilikuwa moja ya vyama vikubwa vya upinzani na Mahdi alisalia kuwa kiongozi mwenye ushawishi.

BREAKING: DIEGO MARADONA AFARIKI DUNIA

Chanzo: millardayo.com