Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri atimba Saudia kufuatia vifo vya wafanyakazi wa Kenya

Waziri Saudua Wafanyakazi.jpeg Waziri atimba Saudia kufuatia vifo vya wafanyakazi wa Kenya

Wed, 2 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa maswala ya kigeni wa Kenya, Alfred Mutua, Jumanne aliondoka nchini humi kuelekea Saudi Arabia kukutana na mamlaka na watu wanaoishi nje ya Kenya ili kukusanya taarifa zaidi kuhusu changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa Kenya katika maeneo ya Ghuba.

Haya yanajiri baada ya habari mwezi uliopita kwamba wanawake 85 Wakenya waliokuwa wakifanya kazi nje ya nchi - wengi wao wakiwa Saudi Arabia - walikuwa wamefariki katika muda wa miezi mitatu iliyopita kulingana na Bw Mutua.

Wanawake wengine 1,000 wa Kenya walikuwa wamerejeshwa makwao, aliongeza.

Safari za Bw Mutua zinakuja baada ya mkutano uliofanyika Jumatatu na wawakilishi wa mawakala wa uajiri ambao huajiri Wakenya kwa kazi nchini Saudi Arabia na maeneo mengine.

Mkutano huo, ambao aliutaja kama "mgumu na ufunuo wa kushangaza", ulikuwa na lengo la kutafuta suluhu za kudumu kwa wafanyakazi wa nje ya nchi.

"Taarifa zilizokusanywa [kutoka kwa maajenti] zinaonyesha hadithi tofauti na ile inayovuma katika vyombo vya habari," Bw Mutua alisema.

Mnamo 2021 wizara ya mambo ya nje ya Kenya ilisema Wakenya 89, wengi wao wakiwa wafanyakazi wa nyumbani, walikufa nchini Saudi Arabia katika miaka miwili iliyopita. Vifo hivyo hata hivyo vilihusishwa na mshtuko wa moyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live