Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri apinga agizo la kubariki ushoga

Mlkss Kuria Waziri apinga agizo la kubariki ushoga

Mon, 25 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria amejiunga na baadhi ya Wakenya kupinga hatua ya Papa Francis wa Kanisa Katoliki kuwaruhusu mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja.

Kwenye ujumbe alioweka kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), Bw Kuria alisema kuwa Kanisa Katoliki nchini halitakubali hata kidogo uhalalishaji wa uhusiano wa kimapenzi wa aina hiyo.

Hata hivyo, Bw Kuria alisema msimamo wake haumaanishi kwamba anamkosea heshima Papa Francis, ambaye ndiye kiongozi wa kanisa hilo kote duniani.

“Msimamo wa Askofu Philip Anyolo kupinga ndoa za jinsia moja ndio wetu sisi sote ambao ni washiriki wa Kanisa Katoliki hapa nchini,” akasema Bw Kuria.

Akaongeza: “Hatutawahi kukubali ndoa za jinsia moja katika kanisa la Kenya. Hili halimaanishi kwamba hatumheshimu Papa.”

Mnamo Jumatatu, Papa Francis aliwaruhusu kirasmi mapadre katika kanisa hilo kuwabariki wanandoa wa jinsia moja.

Kwenye agizo hilo, Papa alisema kuwa mapadre wanaweza kubariki ndoa hizo, ikiwa hafla hizo si sehemu ya ratiba rasmi ya kanisa hilo.

Lakini mnamo Jumamosi, Askofu Anyolo alipinga vikali agizo hilo, akisema kuwa linapinga maagizo ya Mungu kuhusu uhalisia na maana halisi ya ndoa nchini.

Wadadisi wanasema kuna uwezekano agizo hilo la Papa likapata pingamizi zaidi kutoka kwa mataifa tofauti barani Afrika, ambako kanisa hilo lina ufuasi mkubwa. Rayvanny amwaga sababu za kujitoa WCBKrismasi ya masaibu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live