Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri amuaomba msamaha mwandishi muislam kwa kumuita Al-Shabaab

Msamaha Alshabab Waziri amuaomba msamaha mwandishi muislam baada ya kumita Al-Shabaab

Fri, 29 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Elimu Kenya Profesa George Magoha amelazimika kumuomba radhi mwandishi habari wa kike Muislamu wa Televisheni ya NTV baada ya kumfungamanisha na kundi la kigaidi la Al Shabab wiki iliyopita.

Jumatano jioni Magoha alikutana na viongozi wa jamii ya Waislamu nchini Kenya wakiongoziwa na Al Haj Hassan Ole Nado, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Kenya (SUPKEM), ambapo alikutana na mwandishi huyo wa NTV Bi. Rukia Bulle ambapo amemuomba msamaha na pia ameomba msamaha kwa Waislamu na Wakenya kwa ujumla.

Al Haj Ole Naado amewaambia waandishi habari kuwa, baada ya mkutano huo wa maridhiano, Waislamu wameamua kumsahmehe waziri huyo. Naye Abdullahi Abdi Mwenyekiti wa Jukwaa la Waislamu Kenya amesema Waziri Magoha alinyenyekea mbele ya Waislamu na hatua yake ya kuomba asamehewe imekubaliwa. "Ninaamini hatua hiyo ya kuomba radhi ilikuwa ya kweli na ninaomba jamii ya Kiislamu kuikubali. Sisi viongozi tumekubali ombi hilo la kutaka kusamehewa kwa niaba ya mwandishi wa habari na kwa niaba ya Umma," ameongeza.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi kadhaa wa Kiislamu akiwamo Juma Namlola ambaye ni Mwenyekiti wa Waandishi Habari Waislamu nchini Kenya.

Katika video inayoenezwa mitandaoni, Magoha alimuuliza ripota wa kike aliyekuwa amevalia Hijab ikiwa alikuwa anawakilisha kundi la al-shabaab. Mwandishi huyo wa habari alikuwa amemuuliza swali.

“Unamwakilisha nani, ikiwa ni Al Shabaab sitakujibu...,” Magoha alisema. Baraza la vyombo vya Habari Kenya siku ya Jumatano lilidai kwamba Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano imlazimishe Magoha kuomba radhi kwa madai yake ya vitisho vya mara kwa mara dhidi ya wanahabari.

Baraza hilo lilisema ni lazima Magoha awajibike ili kulinda heshima ya waandishi wanaomzungumzia yeye na wizara yake.

"Baraza la vyombo vya habari linatoa wito kwa Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano kuhakikisha waziri anaomba msamaha bila masharti, kuondoa matamshi ya kusikitisha na kubatilisha agizo lake dhidi ya utendakazi mzuri wa vyombo vya habari," taarifa hiyo ilisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live