Cecilia Abena Dapaah aliamini anafanya uamuzi sahihi wa kwenda Polisi kuripoti kuibiwa kiasi kikubwa cha fedha nyumbani kwake lakini kibao kikageuka na kushikiliwa kwa kumiliki kiasi kikubwa cha fedha ambacho kinahusishwa na rushwa.
Inaelezwa ameibiwa Dola Milioni 1 (Tsh. Bilioni 2.4), Euro 300,000 (Tsh. Milioni 812) na Fedha ya Ghana cedis 350,000 (Tsh. Milioni 74), vingine ni begi la mkononi lenye thamani ya Dola 35,000 (Tsh. Milioni 85) na Vito vyenye thamani ya Dola 95,000(Tsh. Milioni 232)
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 68, alitangaza kuachia ngazi lakini amesababisha hasira kwa Wananchi wengi kwa kuwa Fedha ya Ghana imekuwa ikishuka thamani miezi ya hivi karibuni huku ikidaiwa kumekuwa na watu wachache wanaoficha fedha za kigeni.